Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka
Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametangaza rasmi
kuacha kufundisha soka la Tanzania kutokana na maamuzi mabovu katika
baadhi ya michezo ligi kuu Tanzania bara.
“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja
kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana.
Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo
waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya
mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio
kulala kwa bao 1-0 ugenini.
“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli
lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni
kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano
ya kimataifa havifanyi vizuri.”
“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa
Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume
cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu
watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora
nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote
waliokuwa karibu na Julio.”
.png)
0 comments: