Fifa kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia kufikia 48
Rais wa Fifa Gianni Infantino
ameshauri kuongezwa wa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48
zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa
atafikisha timu 40.
Anashauri kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa.
Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.
Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.
''Haya
ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na
kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka
46.
Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.
.png)

0 comments: