Video: Balotelli afanya balaa kama kawaida yake huko Ufaransa
Mario Balotelli kwa sasa anawafunga midomo wote waliokuwa wanasema amekwisha.
Muitaliano huyo alikuwa kwenye wakati mgumu wakati wa majira ya
usajili wa dirisha la kiangazi kutokana na timu nyingi za ligi kubwa za
Ulaya kuonesha hazivutiwi nae hadi mwishowe Nice walipoamua kujitosa
kumchukua kama wanacheza bahati nasibu.
Hadi sasa Balotelli amewalipa kwani tayari ameshafunga magoli 6
kwenye mechi 6, huku goli lake la sita akifunga dakika za lala salama
wakati timu yake ikipata ushindi dhidi ya Lorient.
Lakini Balotelli anabaki kuwa Balotelli tu, amejikuta analambwa kadi nyekundu baada ya kugombana na mchezaji wa Lorient.
Awali alioneshwa kadi ya njano baada ya kushangilia goli lake kwa
kuvua jezi kisha akaoneshwa kadi ya pili ya njano muda mfupi kutokana
na tukio la kuoneshana ubabe na mchezaji wa Lorient ambapo anaonekana
kama alimpiga kichwa licha ya tukio hilo kuonekana kama ni jepesi
ukilinganisha na adhabu.
Goli alilofunga Mario Balotelli dhidi ya Lorient
.png)
0 comments: