Arsenal kumtoa Jack Wilshere kwa mkopo
Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo
kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika
katika kikosi cha kwanza cha timu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu
aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha
hilo.
Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita
,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa
katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.
Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu.
.png)
0 comments: