Fifa kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia kufikia 48



Rais wa Fifa Gianni Infantino ameshauri kuongezwa wa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48 zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa atafikisha timu 40.

Anashauri kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa.

Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.
Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.

''Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka 46.

Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.

Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka

dsc_0247

Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametangaza rasmi kuacha kufundisha soka la Tanzania kutokana na maamuzi mabovu katika baadhi ya michezo ligi kuu Tanzania bara.

“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio kulala kwa bao 1-0 ugenini.

“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri.”

“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”

Video: Balotelli afanya balaa kama kawaida yake huko Ufaransa

mario-balotelli

Mario Balotelli kwa sasa anawafunga midomo wote waliokuwa wanasema amekwisha.

Muitaliano huyo alikuwa kwenye wakati mgumu wakati wa majira ya usajili wa dirisha la kiangazi kutokana na timu nyingi za ligi kubwa za Ulaya kuonesha hazivutiwi nae hadi mwishowe Nice walipoamua kujitosa kumchukua kama wanacheza bahati nasibu.

Hadi sasa Balotelli amewalipa kwani tayari ameshafunga magoli 6 kwenye mechi 6, huku goli lake la sita akifunga dakika za lala salama wakati timu yake ikipata ushindi dhidi ya Lorient.

Lakini Balotelli anabaki kuwa Balotelli tu, amejikuta analambwa kadi nyekundu baada ya kugombana na mchezaji wa Lorient.

Awali alioneshwa kadi ya njano baada ya kushangilia goli lake kwa kuvua jezi kisha akaoneshwa kadi ya pili ya njano muda  mfupi kutokana na tukio la kuoneshana ubabe na mchezaji wa Lorient ambapo anaonekana kama alimpiga kichwa licha ya tukio hilo kuonekana kama ni jepesi ukilinganisha na adhabu.

Goli alilofunga Mario Balotelli dhidi ya Lorient
 
 
 

Hatimaye Timu ya Serengeti Boys imefuzu michuano ya Afrika...!!



Timu ya vijana wa Tanzania chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) leo wamejihakikishia safari ya kushiriki michuano ya Afrika baadaya ya kutoka sare kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Timu ya vijana Congo Brazzavile. Awali mechi ya awali ambayo Timu ya Vijana ya Tanzania Serengeti Boys wakiwa nyumbani, walishinda 3 -2 dhidi ya timu hiyo ya Congo na hivyo kwa ushindi wa leo Vijana hao wamefuzu michuano hiyo.

Kabla ya kuwaondoa vijana wa Congo Brazzavile, vijana hao wa Serengeti Boys waliwaondoa timu ya Afrika Kusini.

Manchester City yalazwa na Tottenham


Klabu ya Whitehart Lane nchini Uingereza Tottenham Hotspurs iliisitisha rekodi ya Manchester City ya kutofungwa.

Goli la kujifunga wenyewe la Aleksander Kolarov liliiweka Tottenham kifua mbele baada ya kuichanganya krosi ya Danny Rose alipokuwa akijaribu kuokoa na hivyobasi mpira kumpita kipa Claudio Bravo.

Dele Ali aliongeza bao la pili ndani ya eneo hatari la City kufuatia pasi nzuri ya Son Heung-min.

Spurs walipata penalti wakati Ali Dele alipoangushwa na Fernandinho katika lango la Manchester City,lakini Bravo aliokoa mkwaju wa Erik Lamela.

Hali Tete kwa Morinho



Hali ya Kocha wa Manchester United imeendelea kuwa tata baada ya hii leo kupata matokeo yasiyoridhisha. Leo Manchester United ilishuka dimbani kukipiga na timu ya Stock City huku wakilazimishwa sare ya 1 - 1. Tangu msimu huu uanze imekuwa shida kwa upande wa Manchester United baada ya kuwa na kocha mwenye rekodi nzuri katika soka lakini pia wachezaji wake ambao wamesajiliwa kwa gharama kubwa hususani Pogba ambaye amevunja rekodi ya dunia lakini hadi kufikia sasa bado imekuwa ngumu kwa upande wake kubeba kikosi hiko na kudhihirisha ubora na gharama iliyotumika.

Arsenal kumtoa Jack Wilshere kwa mkopo

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Jack Wilshere

Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika katika kikosi cha kwanza cha timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha hilo.
 
Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita ,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.

Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu.