Manchester City yalazwa na Tottenham
Klabu ya Whitehart Lane nchini Uingereza Tottenham Hotspurs iliisitisha rekodi ya Manchester City ya kutofungwa.
Goli
la kujifunga wenyewe la Aleksander Kolarov liliiweka Tottenham kifua
mbele baada ya kuichanganya krosi ya Danny Rose alipokuwa akijaribu
kuokoa na hivyobasi mpira kumpita kipa Claudio Bravo.
Dele Ali aliongeza bao la pili ndani ya eneo hatari la City kufuatia pasi nzuri ya Son Heung-min.
Spurs
walipata penalti wakati Ali Dele alipoangushwa na Fernandinho katika
lango la Manchester City,lakini Bravo aliokoa mkwaju wa Erik Lamela.
.png)

0 comments: